HISTORIA YA KANISA
Kanisa la Mwanga nimoja ya Makanisa saba (7) katika mtaa wa North Pare. Mtaa ambao wainjilisti wa kwanza walifika miaka 80 iliyopita. Licha ya wamisionari wa kwanza wasabato kuingia mwaka 1902 katika milima ya upare, bado eneo la mtaa wa North Pare linajulikana kama eneo jipya katika dini ya Wasabato.
MTIZAMO WA VIONGOZI WA NETCOViongozi wa NETCO bado wanalitizama eneo hili kwa jicho la upendeleo licha yakuwa na washiriki wachache, ila msukumo mkubwa upo katika Kanisa la Mwanga lenye washiriki wapatao 189.
CHIMBUKO LA UJENZI WA KANISA


Chimbuko la ujenzi wa kanisa la Mwanga ni neno DESIRE (Shauku) maana halisi ni "The starting point of all achievements" 

SHULE YA SABATO
Idara ya shule ya sabato ilianza mwaka 1852 miaka 10 kabla ya kanisa la ulimwengu kupangwa kuwa kanisa lenye mfumo mwaka183. Shule ya sabato ni mfumo wa kanisa mahalia wa kujifunza kumfahamu Mungu na kulea waumini -Ina shughulika kujenga imani mahusiano kati ya Mungu na muumini -Inajenga matendo ya waumini kupitia matumizi ya kanuni za Biblia tunazojifunza toka katika Biblia -Shule ya sabato inayo malengo manne,ambayo ndiyo mhimili wa kuendeshesha shule ya sabato.

1.KUJIFUNZA BIBLIA- Neno laMungu. Lengo lenye makusudi ya kujilisha kwa neno, kuipa afya ya Akili nakuboresha maisha ya muumini na Mungu wake.(Yoh 17:3)

2.USHIRIKIANO. Hapa ni kuboresha mahusiani kati ya muumini na muuminii (Matend 2:44-45).Eneo hili ndipo umaana wa vikosi vya shule ya sabato vya watu sita hadi nane ni lazima kwa kila kusanyiko la waadventista wasabato.Vikitumika kama inavyotakiwa katika Nyanja zake zote uboresha mahusiano ya wauini na Mungu wao na wao kwa wao.Ujenga umoja miongoni mwa waumini kila mmoja kwa mwenzio.

3.HUDUMA KWA JAMII. Eneo hili ni kumfanya muunini kuwa mtenda kazi pamoja Mungu, kwa waumini wa ndani na nje.- Kutambua mahitaji ya wenzetu, waliyo ndani na nje na kuyashughulikia. Katika sehemu hii kila kikosi kina hitaji kutambua mazingira yake na mahitaji .Hapa mbinu za Yesu za kuwafikia watu zinapaswa kutumika.Hapa kila muumini aliye ndani ya kanisa anapaswa kuifikia jamii iliyo nje ya kanisa. Kuifanya jamii hiyo iwe wanafunzi wa Yesu. -Inalenga kufikia wakazi waliyo maeneo ya kanisa na nje ya kanisa - Ibada ya matoleo hapa ni sehemu yake ,waumini kutoa zaka ,sadaka na sadaka za hiari.Kila muumini analazimika kutoa mali zake talanta zake muda wake kuwafikia watu na injili ya Yesu mfufuka Shule ya sabato ni chombo pekee cha kuongoa roho ,kulea na kuimarisha imani za waumini- nichombo cha Umishenari .Kila kanisa linalazimika kukiboresha na kukiendesha kama ilivyo kusudiwa kukamilisha utume